EDK: FORM ONE
- MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA DINI.
- Mtazamo wa Kikafiri juu ya Dini.
- Kafiri Mutlaq ni yule anayekanusha moja kwa moja kinadharia na kivitendo kuwepo kwa Allah (s.w), maamrisho yake, vitabu vyake na mitume wake.
- Kwa mtazamo wa Kikafiri, neno ‘Dini’ lina maana zifuatazo;
- Ni imani juu ya kuwepo Mungu Muumba.
“Belief in the existence of a supernatural ruling power…” (English Dictionary)
- Ni imani inayohusiana na mambo ya kiroho baina ya binaadamu na Mwenyezi Mungu.
-
- Dhana ya Dini kwa mujibu wa Qur’an.
- Maana ya Dini kwa mtazamo wa Qur’an (Uislamu).
- Dhana ya Dini kwa mujibu wa Qur’an.
- ‘Dini’ ni neno la kiarabu lenye maana zifuatazo;
- Itikadi na njia ya maisha.
- Uwezo au mamlaka au utawala.
- Mila au mfumo wa maisha unaofuatwa na jamii ya watu.
- Siku ya malipo (mfumo wa maisha ya Akhera).
Rejea Qur’an (3:83).
- Kwa ujumla ‘Dini’ maana yake ni mfumo au utaratibu wowote wa kuendeshea kila kipengele cha maisha unaofuatwa na jamii fulani ya watu.
-
-
- Aina kuu za Dini.
-
- Kuna aina kuu mbili za dini hapa ulimwenguni;
- Dini ya Allah (s.w).
- Dini za wanaadamu.
- Dini ya Allah (s.w).
- Ni Uislamu ambao ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata kikamilifu muongozo wa Allah (s.w).
- Dini za Watu (wanaadamu).
- Ni mifumo ya kuendeshea maisha iliyowekwa na wanaadamu inayotokana na matashi yao.
-
-
- Makundi ya Dini za wanaadamu (watu):
-
Dini za wanaadamu zimegawanyika makundi makuu matatu;
- Dini ya Ukafiri
– Ni utaratibu wa maisha ulioundwa katika misingi ya kukanusha muongozo wa Allah (s.w) na Mitume wake.
- Dini ya Ushirikina
– Ni utaratibu wa maisha uliofumwa katika misingi ya kumshirikisha Allah (s.w) na miungu wengine.
- Dini ya Utawa
– Ni utaratibu wa maisha ambao wafuasi wake hujitenga mbali vitu vizuri na harakati za kumletea mwanaadamu maendeleo hapa ulimwenguni.
-
-
- Maana ya Al-Islam (Uislamu).
-
Al-Islam - ni jina la Dini ya Allah (s.w) lenye maana zifuatazo:
- Mwenendo mwema au kujisalimisha moja kwa moja au kutii kwa unyenyekevu sheria, maagizo au maamrisho ya Muumba.
- Uislamu ni utaratibu wa maisha unaofuata bara bara mwongozo wa Allah (s.w) na Sunnah ya Mitume wake.
Rejea Qur’an (3:83), (30:30).
- Ni neno lenye maana ya ‘salama’ kwa maana ya amani.
- Uislamu ni dini ya amani.
- Ni utaratibu wa maisha unaoendeshwa kwa kujisalimisha kwa Allah (s.w) kwa kufuata kikamilifu sheria zake.
- Ni utaratibu (mfumo) pekee ndio unaoweza kuleta furaha na amani ya kweli kwa maisha ya binfsi ya kijamii pia.
-
-
- Nani Muislamu.
-
- Ni yule anayemnyenyekea Allah (s.w) kwa kufuata kikamilifu sheria na kanuni zake zote.
- Ni yule anayeishi maisha yake yote kwa kuchunga bara bara mipaka ya Allah (s.w) kwa kufanya yale yote aliyoamrishwa na kuacha yote aliyokatazwa kwayo.
Rejea Qur’an (2:208), (3:102).
Zoezi la 3.
- Nini maana ya neno ‘Dini’ kwa mtazamo wa,
-
- Kikafiri.
- Kiislamu.
-
- (a) Bainisha dini kubwa hapa Ulimwenguni.
(b) Taja makundi ya dini za wanaadamu.
- “Je! Wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kimejisalimisha kwake kipende kisipende………” (3:83).
Kwa kwa kuzingatia aya hii toa mafunzo mawili (2) yanayohusiana na Dini.
- (a) Toa maana mbili za neno “Islam”
(b) Nani muislamu?